August 23, 2015

WAPAMBANAJI WA MABADILIKO TABIA NCHI








By Rahim Nasser

WAPAMBANAJI WA MABADILIKO TABIA NCHI

  Mtandao wa vijana wanaharakati wa maadiliko tabia nchi ni kundi la vijana shupavu wenye uweledi na uelewa wa mabadiliko tabia nchi, ulioundwa kupambana na kuelimisha umma juu ya wajibu wao kuhusu mabadilikotabia nchi. Dunia ipo hatarini na wengi wanahofia vita, ujangili, siasa na mambo yafananayo na hayo yanayomhusu binadamu na mazingira anayoishi, ila kuongezeka kwa joto kidunia ni tishio kubwa la uhai kuliko hata vita ya kwanza na ya pili, mvua zinazozidi ama kupungua kwa baadhi ya maeneo huleta majanga, kiangazi kikizidi hua maafa, majangwa yanaongezea urefu na upana lakini watu hawajishughulishi na kimya wanatazamana.

Hapo ndipo vijana hawa wapambanaji wanaingia katika jamii na katika maofisi ya viongozi wa kiserikali na wasiokiserikali kuhamasisha na kuelimisha juu ya mabadiliko tabia nchi. Jamii imezungukwa na wakulima na wafugaji, wasomi na wafanyakazi na makundi yote haya ni muhimu  kwa vijana hawa katika utoaji elimu, wanafuzi wote wa masekondari, elimu ya juu na hata ile ya msingi wanafikiwa kwa uwepo wa vilabu chungumzima vilivyotapakaa nchini huku wafanayakazi wanafikiwa kwa semina na matamasha mbalimbali na wakati wakulima na wafugaji wanafikiwa kwa misafara inayotengenezwa  kufikia vijiji na mikaoa kadha wa kadha.


Kila Nyanja inayohusu mwanadanu yenye na mahusiano na mabadiliko tabia ya nchi mathalan utawala bora, uchumi, utalii, madini, maradhi nakadhalika vijana hawa hushiriki kuhamasisha usawa wa kimaslahi, haki na wajibu kati mtenda na mtendwa katika kutendeana. Ni ukweli usiopingika kuwa pasipo na utawala bora panarushwa na rushwa niadui wa haki, penyerushwa vyazo vya maji vitaharibiwa, penye rushwa madini yatachotwa bila mpangilio na kuachwa mashimo makubwa na manene, penye rushwa vyombo vya moto chakavu vyenye kutoa moshi mchafu na viwanda vilivyochini ya viwango vyenye kuharibu mazingira na kuchangia mabadiliko tabia nchi na uharibifu wa mazingira vitaendelea kufanya kazi, pasipo utawala bora mataifa yenye nguvu yataendekeza sikio la kufa juu ya mabadilikko tabia nchi na majanga yanayo ikumba dunia.

Lakini pia shughuli za kiuchumi na kiutalii zisipo angaliwa kwa jicho la tatu zinaweza kuathir zaidi mazingira na kuchangia mabadiliko tabia nchi, ukataji na uvunaji wa miti misituni kwa shughuli za kiuchumi, kupata nishati, ujenzi na fedha bila kupanda upya miti mingine kunachangia ukame na uharibifu wa makazi ya wanyama na ndege pamoja na vyanzo vya maji, vijana hawa wanaharakati wanajumnika na jamii hizi kuzihamasisha na kuzipa elimu juu ya njia mbadala za kujikwamua kiuchumi na matumizi bora ya nishati ikiwemo uwazinshwaji wa vikoba na matumizi ya mkaa mbadala pasi na kuacha upandaji wa miti ikuayo kwa kasi na yenye kuastahimili ukame. 

Juhudi zote hizi zinazofanywa na mtandao huu shukran kubwa zinaenda kwa shirika la misaada ya kimakanisa la Norway, hawa ni washirika na wadhamini wa kwanza wa vijana hawa na kwa kupitia washirika wengine wa washirika hili kutoka dini mbalimbali vijana hao wanaweza kushiriki program tofauti tofauti za kimaendeleo .

Shirika hili la misaada ya kimakanisa la Norway likishirikiaana na asasi zingine tofauti ndio waasisi wa mtandao huu zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Ndani ya mdaa huu mtandao huu umeshuhudia  mafaniko makubwa wa shughuli zake kijamii. 

Mbali na mafanikio kuna changamoto, japo changamoto si sawa  na matatizo,  utofauti wake nikuwa changamoto zinatatulika kirahisi zaid kuliko matatizo, wakati mwengine nikipata wasaa nitazungumzia zaidi fursa , mafanikio na changamoto zilizopo katika mtandao huu ufahamikao kwa lugha ya kigeni kama Youth Climate Activist Network (YouthCAN ) mpaka wakati huo.
Mungu inusuru Dunia, Mungu bariki mtandao wa vijana wanaharakati (YouthCAN Tanzania).

Published By
Media and Communication Department

July 24, 2015



I will Go by Bike!

By BARAKA K. CHEDEGO
 


Today I have decided about this journey to rescue,
I afraid to shut my mouth up while situation is at due,
Toleration is the greatest gift of mind but I’m tired to be fool,
My plan is to go by bike and I won’t care about you.

By this idea of bike some may think I’m insane,
But to show how I mean, in this I won’t use plane,
I will ensure that people know what I claim,
Because having a just world have been my lifetime dream.

Natamani niongee Kiswahili ili na nyumbani wanielewe,
Amba nali nonje chigogo lunji wa kukaya wasechelele,
Mais l’affaire ci a bosium de l’union international,
Ce pour cela les francais mout permis de s’exprimer en englais.

Climate has touched gender issues in my city,
Now as I’m speaking Malaria is chewing Africa because of climate,
Trachoma is the song sung when water is scarce,
Skin cancer the son of Global Warming has got a chance.

Isimo seZulu sishintshile na kwaZulu- Natal,
Isimo sinzima kakhulu kwi ningizimu Africa,
But the police of the world act like they don’t see,
When I say is human forces they don’t agree.
Personally I don’t agree that East and West can’t get along,
I don’t agree that right is Wright and left is long,
If for people to understand it will need me to sing a song,
I will sing the beautiful one entitled “I will Go by Bike”

This is not only the issue of environment,
It touches gender, culture and even security,
Its an issue of economy, technology and even politics,
That’s what gives me a reason to speak instead of keeping quite.

I will repair my bike for this Paris road to speak my concern,
I won’t hesitate to share with my partners in COP 21,
If we will fail to maintain life in Earth living planet,
We will never manage in dead planet like Mars.

                                                                                  Published by 
                                                                                      Media and communication Department


December 21, 2014

CONGRATULATIONS TO OUR NEW LEADER, FRANCISCA DAMIAN MBOYA (IRON LADY) 2015/2016



Smilling, is Fransisca Damian Mboya.  New 2015 YouthCAN Coordinator.
 Justne Mponda, previous coordinator

VIJANA WA YOUTHCAN KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI WA VIONGOZI MWAKA 2015

 Fadhil Meta akinadi sera kwa wajumbe wa uchaguzi wa viongozi wa YouthCAN
 Fadhil Meta akijibu maswali ya wajumbe
 Wagombea wengine Smart Deus pamoja na Fransisca Damiani wakimsikiliza mgombea mwenzao Fadhil Meta
 Fransisca Damian akinadi sera zake katika ukumbi wa mkutano mbele ya wajumbe

 Fransisca Damian akijibu maswali kutoka kwa wajumbe wa uchaguzi
 Smart Deus, mgombea wa tatu akisikiliza kwa makini sera za mgombea mwenzake


 Smart Deus akinadi sera zake kwa wajumbe wa mkutano
Wagombea Fransisca Damian pamoja na Fadhil Meta wakisikiliza kwa makini sera za mgombea mwezao

December 14, 2014

PICHA ZA MAENEO AMBAYO VIJANA WA YOUTH CAN WALIPETA NA KUWEZA KUONA JINSI GANI SHUGHULI ZA UVUNAJI WA MBAO UNAVYOCHANGIA KUARIBU MAZINGIRA NA WALIWEZA KUKUTANA NA MKUU WA WILAYA YA CHUNYA KATIKA SAFARI YAO YA KUHAMASISHA WATU KUTUNZA MAZINGIRA

shuguli za uvunaji wa mbao jinsi unanyoathiri mazingira katika taifa letu
 Mbao zilizokwisha kuvunwa kutoka katika misitu mkoani mbeya zikiwa tayari kwa kusafirishwa
 Mkuu wa wilaya ya Chunya akihutubia wajumbe walihuzuria mkutano wa mazingira
 Mkuu wa wilaya Chunya akiweka saini katika madai ya haki kutoka kwa vijana wa YouthCAN Tanzania

Uchimbaji wa madini jinsi unavyoharibu mazingira katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya

HATIMAYE VIJANA WA YOUTH CAN WAFANYA TAMASHA KUBWA LA MAZINGIRA KATIKA VIWANJA VYA DON BOSCO UPANGA.TAZAMA PICHA ZA MATUKIO YA TAMASHA LA MAZINGIRA


 VIJANA KUTOKA GNRC WAKIIMBA NYIMBO ZA MAZINGIRA KATIKA TAMASHA LA YOUTH CAN
 WANAFUNZI WALIOSHIRIKI TAMASHA HILO WAKISIKILIZA KWA MAKINI KILICHOKUWA KINAENDELEA
 MEZA KUU YA MGENI RASMI NA VIONGOZI WA NCA WAKITIZAMA BURUDANI ILIYOKUWA IKITOLEWA NA VIJANA WA YOUTH CAN
 VIJANA WAKIFUATILIA KILICHOKUWA KINAENDELA KWA TAMASHA HILO
 TAMASHA KWELI LILIKUWA NA WATU WENGI
 WANAFUNZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM WAKIFUATILIA KWA MAKINI KILICHOKUWA KINAENDELEA KWA TAMASHA LA MAZINGIRA
HATIMAYE VIONGOZI WA CLUB BORA ZA MAZINGIRA WALIWEZA KUPEWA ZAWADI KWA KAZI NZURI ZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KATIKA SHULE ZAO

November 24, 2014

YOUTH CAN WAKIWA KATIKA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MSAFARA WA MAZINGIRA KATIKA MIKOA YA MBEYA PWANI PAMOJA NA IRINGA WAKITOA ELIMU KUHUSU MABADILIKO YA TABIA NCHI

 Wanafunzi wa mkoa wa Njombe wakieleza kitu kuhusu mabadiliko ya tabia nchi baada ya mafunzo kutoka kwa vijana wa Youth CAN

 Wanafunzi wa sekondari mkoa wa Njombe wakisaini madai ya haki baada ya kupata elimu kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi
 Wanafunzi mkoani Njombe wa shule maalumu ya viziwi wakisikiliza kwa umakini mafunzo ya mazingira kutoka kwa vijana wa Youth CAN
 Vijana wa mkoa wa Pwani wilaya ya Bagamoyo wakisaini madai ya haki kuhusu uharibifu wa mazingira yaliyotolewa na vijana wa Youth CAN
 Vijana wa Youth CAN wakitoa burudani ya nyimbo za mazingira kwa wakazi wa mkoa wa Pwani wilayani Bagamoyo
 Vijana wa mkoa wa Bagamoyo wakifuatilia  kwa umakini mada za mazingira kutoka kwa vijana wa Youth CAN
Mwanakijiji wa kijiji cha Msata wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani akielezea jinsi gani walivyoathirika na mabadiliko ya tabia nchi

Translate