August 23, 2015

WAPAMBANAJI WA MABADILIKO TABIA NCHI








By Rahim Nasser

WAPAMBANAJI WA MABADILIKO TABIA NCHI

  Mtandao wa vijana wanaharakati wa maadiliko tabia nchi ni kundi la vijana shupavu wenye uweledi na uelewa wa mabadiliko tabia nchi, ulioundwa kupambana na kuelimisha umma juu ya wajibu wao kuhusu mabadilikotabia nchi. Dunia ipo hatarini na wengi wanahofia vita, ujangili, siasa na mambo yafananayo na hayo yanayomhusu binadamu na mazingira anayoishi, ila kuongezeka kwa joto kidunia ni tishio kubwa la uhai kuliko hata vita ya kwanza na ya pili, mvua zinazozidi ama kupungua kwa baadhi ya maeneo huleta majanga, kiangazi kikizidi hua maafa, majangwa yanaongezea urefu na upana lakini watu hawajishughulishi na kimya wanatazamana.

Hapo ndipo vijana hawa wapambanaji wanaingia katika jamii na katika maofisi ya viongozi wa kiserikali na wasiokiserikali kuhamasisha na kuelimisha juu ya mabadiliko tabia nchi. Jamii imezungukwa na wakulima na wafugaji, wasomi na wafanyakazi na makundi yote haya ni muhimu  kwa vijana hawa katika utoaji elimu, wanafuzi wote wa masekondari, elimu ya juu na hata ile ya msingi wanafikiwa kwa uwepo wa vilabu chungumzima vilivyotapakaa nchini huku wafanayakazi wanafikiwa kwa semina na matamasha mbalimbali na wakati wakulima na wafugaji wanafikiwa kwa misafara inayotengenezwa  kufikia vijiji na mikaoa kadha wa kadha.


Kila Nyanja inayohusu mwanadanu yenye na mahusiano na mabadiliko tabia ya nchi mathalan utawala bora, uchumi, utalii, madini, maradhi nakadhalika vijana hawa hushiriki kuhamasisha usawa wa kimaslahi, haki na wajibu kati mtenda na mtendwa katika kutendeana. Ni ukweli usiopingika kuwa pasipo na utawala bora panarushwa na rushwa niadui wa haki, penyerushwa vyazo vya maji vitaharibiwa, penye rushwa madini yatachotwa bila mpangilio na kuachwa mashimo makubwa na manene, penye rushwa vyombo vya moto chakavu vyenye kutoa moshi mchafu na viwanda vilivyochini ya viwango vyenye kuharibu mazingira na kuchangia mabadiliko tabia nchi na uharibifu wa mazingira vitaendelea kufanya kazi, pasipo utawala bora mataifa yenye nguvu yataendekeza sikio la kufa juu ya mabadilikko tabia nchi na majanga yanayo ikumba dunia.

Lakini pia shughuli za kiuchumi na kiutalii zisipo angaliwa kwa jicho la tatu zinaweza kuathir zaidi mazingira na kuchangia mabadiliko tabia nchi, ukataji na uvunaji wa miti misituni kwa shughuli za kiuchumi, kupata nishati, ujenzi na fedha bila kupanda upya miti mingine kunachangia ukame na uharibifu wa makazi ya wanyama na ndege pamoja na vyanzo vya maji, vijana hawa wanaharakati wanajumnika na jamii hizi kuzihamasisha na kuzipa elimu juu ya njia mbadala za kujikwamua kiuchumi na matumizi bora ya nishati ikiwemo uwazinshwaji wa vikoba na matumizi ya mkaa mbadala pasi na kuacha upandaji wa miti ikuayo kwa kasi na yenye kuastahimili ukame. 

Juhudi zote hizi zinazofanywa na mtandao huu shukran kubwa zinaenda kwa shirika la misaada ya kimakanisa la Norway, hawa ni washirika na wadhamini wa kwanza wa vijana hawa na kwa kupitia washirika wengine wa washirika hili kutoka dini mbalimbali vijana hao wanaweza kushiriki program tofauti tofauti za kimaendeleo .

Shirika hili la misaada ya kimakanisa la Norway likishirikiaana na asasi zingine tofauti ndio waasisi wa mtandao huu zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Ndani ya mdaa huu mtandao huu umeshuhudia  mafaniko makubwa wa shughuli zake kijamii. 

Mbali na mafanikio kuna changamoto, japo changamoto si sawa  na matatizo,  utofauti wake nikuwa changamoto zinatatulika kirahisi zaid kuliko matatizo, wakati mwengine nikipata wasaa nitazungumzia zaidi fursa , mafanikio na changamoto zilizopo katika mtandao huu ufahamikao kwa lugha ya kigeni kama Youth Climate Activist Network (YouthCAN ) mpaka wakati huo.
Mungu inusuru Dunia, Mungu bariki mtandao wa vijana wanaharakati (YouthCAN Tanzania).

Published By
Media and Communication Department

No comments:

Post a Comment

Translate